RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
`
Udhamini wa Umma
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

Chini ya Sheria ya Mdhamini wa Umma Sura ya 31 Toleo la 2002 Kabidhi Wasii Mkuu/RITA ni msimamizi wa  mali yeyote baada ya kubainika kuwa mali hiyo haina mwenyewe au chombo kilichokuwa kinaishikilia mali hiyo kimetoweka. Pia Kabidhi Wasii Mkuu/RITA ana jukumu la kusimamia maslahi/mali au hisa za mtoto aliye chini ya umri wa miaka 18 baada ya kubaini kuwa hakuna jamaa aliye tayari kuwa mlezi guardian wa mtoto huyo ili ashikilie hisa/mali zake, mpaka hapo mtoto huyo atakapofikisha umri wa utu uzima na kukabidhiwa hisa/mali zake.

Sheria ya Mdhamini wa Umma yaani The Public Trustee (Powers and Function) Act; Appointments inamtaja Kabidhi Wasii Mkuu kuwa ni Mdhamini wa Umma.

1: Bila Uteuzi wa Mahakama

  • Kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (1) (a) cha Sheria ya Mdhamini wa Umma Kabidhi Wasii Mkuu anaweza kuendelea kusimamia mali isiyo na mwenyewe moja kwa moja bila kuteuliwa na Mahakama.
  • Vilevile Sheria ya Muunganisho wa Wadhamini, Sura ya 318, Kifungu cha 23 (1) na (2) Kabidhi Wasii Mkuu kama Mdhamini wa Umma anaweza kushikilia mali za Bodi ya Wadhamini baada ya kuifuta bila kuteuliwa na Mahakama.


2: Kwa Uteuzi wa Mahakama

Kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (1) (b) na 7 cha Sheria ya Mdhamini wa Umma Kabidhi Wasii Mkuu anaweza kuomba kuteuliwa kuwa Mdhamini na Mahakama yenye mamlaka kwa kufuata taratibu zifuatazo:-

  • Kumjulisha Mwanasheria Mkuu juu ya kuwepo na mali ya umma isiyo na mmiliki, au inayoelekea kukosa mmiliki.
  • Mwanasheria Mkuu atapeleka maombi Mahakama Kuu chini ya Sheria ya Mdhamini wa Umma Sura ya 31 toleo la 2002.
  • Mdhamini wa Umma atateuliwa kusimamia mali hadi maagizo zaidi ya mahakama au mtu aliyepangwa atakapojitokeza.
Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu