Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Abdul-razaq Badru amesema hii leo jijini Dar es salaam kuwa Wanafunzi wapya zaidi ya 40,000
na wanaoendelea na masomo wapatao 80,000 kwa mwaka wa masomo 2018/2019 watapatiwa mikopo ambapo zaidi ya shilingi bilioni 427 zimetengwa kwa ajili hiyo na kwamba wanafunzi wasiwe na hofu wahakikishe wanakamilisha kwa usahihi ujazaji wa fomu pamoja na nyaraka muhimu zinazohitajika kuanzia leo tarehe 10 Mei hadi julai 15 mwaka huu.