Mkoa wa Mara na Simiyu inatarajia kuanza utekelezaji wa mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 734,357 ambapo Mkoa wa Mara Watoto 383507 na Simiyu Watoto 351850. Mpango huo utaanza mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu.
Tayari maandalizi yote yamekamilika ikiwemo mafunzo maalum ya siku moja yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwa viongozi wa Mikoa hiyo yaliyojumuisha Wakuu wa Wilaya zote, Wakurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wa Idara ya afya na maendeleo ya Jamii.