RITA YAVUKA MALENGO USAJILIWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA MITANO KWA MKOA WA NJOMBE NA IRINGA.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy Hudson akiongea na Waandishi wa Habari hii leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya Mpango wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa Mkoa wa Njombe na Iringa, kulia kwake ni Mkurugenzi wa TEHAMA Bw Cuthbert Simalenga na Kushoto kwake ni Meneja Usajili wa Vizazi ,Vifo Ndoa na Talaka Bi Angela Anatory.
Kwa mujibu wa takwimu tangu mpango huo uzinduliwe kwa Mikoa hiyo miwili mnamo tarehe 22 Septemba 2016 hadi sasa ni asilimia 98% kutoka asilimia 8.5% ya awali kwa Mkoa wa Njombe na Iringa kutoka asilimia 11.7% na kufikia asilimia 95% ndani ya kipindi kifupi.