Wananchi wametakiwa kufuatilia vyeti vya kuzaliwa vya Watoto wao ndani ya siku 90 mara baada ya Mtoto kuzaliwa ili kuepukana na msongamano unaosababishwa na uharaka wa cheti hicho pindi kinapohitajika sehemu mbalimbali za huduma za kijamii ikiwemo bima ya afya na Mamlaka za ajira.
Kwa upande wa watu wazima na vijana ambao hawana vyeti vya kuzaliwa ni vizuri kuanza mapemba taratibu za maombi ya usajili na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kabla havijahitajika kwa matumizi mbalimbali.
Ni kawaida kila mwaka kuwa na kundi kubwa la vijana kutoka vyuo mbalimbali na shule za sekondari wanaohitaji kujiunga na masomo au kuomba ajira na hivyo kukosa nyaraka hiyo muhimu na kusababisha wengi wao kuhitaji kwa haraka hali inayosababisha msongamano katika ofisi za RITA kote Nchini ikiwemo Makao Makuu Jijini Dar es salaa.