Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chna amesema kuwa Watoto zaidi ya milioni 8.8, wamesajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa katika mikoa 26 ya Tanzania bara kupitia Mpango wa Usajili wa Watoto wa Umri chini ya miaka mitano.
Mhe. Waziri Balozi Dkt. Pindi Chana ameyasema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango leo Disemba 08,2023 katika viwanja vya Mbagala Zakhiem Jijini Dar es Salaam.