Naibu Kaibidhi Wasii Mkuu Bi. Irine Lesulie amefungua mafunzo ya siku moja kwa Wafanyakazi wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) kuhusu mfumo mpya wa upimaji na usimamizi wa utendaji kazi wa kila mtumishi na taasisi katika utumishi wa umma unaojulikana kama PEPMIS kwa upimaji wa watumishi na PIPMIS kwa upande wa Taasisi za Umma.
Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika mwishoni mwa juma katika ofisi za RITA Makao Makuu Jijini Dar es salaam yakiratibiwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, UTUMISHI.
Ikumbukwe hapo awali Serikali ilikuwa ikitumia mfumo wa wazi wa mapitio na upimaji wa utendaji kazi (OPRAS) kusimamia utendaji kazi wa watumishi wa umma lakini kutokana na changamoto zake imeamua kuja na mfumo mpya ambao utajibu changamoto za mfumo wa OPRAS.