RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
Album Detail
June
16
2022
Siku ya Mtoto wa Afrika 2022
News Update
Dar es Salaam



`
Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika ni matokeo ya Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990 kwa lengo la kumbukizi ya Watoto wa Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini waliouawa mnamo tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi. Watoto hao walikuwa wakidai haki zao za kutobaguliwa sambamba na haki nyingine za msingi za binadamu ikiwemo haki ya kupata elimu bora huku wakipinga mifumo ya elimu ya kibaguzi. Ili kuwakumbuka na kuunga mkono madai ya haki za watoto hao, OAU iliazimia kuwa tarehe 16 Juni kila mwaka iwe siku maalum ya kumbukizi ya Mtoto wa Afrika. Je umempatia mtoto wako haki yake ya kutambuliwa kwa kusajiliwa na kupatiwa cheti cha kuzaliwa? Kama tayari hongera kwa kutimiza wajibu wako na kama bado basi hujachelewa fanya hivyo ili Mtoto wako atimize ndoto katika maisha yake hapo baadaye kwa kumfungulia fursa ya elimu,matibabu na ajira.
View Full Page