''Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu ni suala la msingi katika mifumo ya kisiasa na ya utawala bora na unasaidia kujumuisha jamii katika maamuzi, kulinda haki za binadamu, kuhakikisha huduma za jamii muhimu zinawafikia wananchi na pia kuleta uwiano sawa katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii''.Alisema Waziri wa Katiba na Sheria Mhe, Balozi. Dkt Augustine Mahiga katika maadhimisho ya siku ya Usajili wa Matukio Muhimu ya Binadamu na Takwimu yaliyofanyika hii leo barani Afrika ambapo kwa Tanzania yameadhimishwa katika chuo cha Sheria jijini Dar es salaam.