Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma amewataka Wanasheria wa Serikali kuhakikisha wanatumia ujuzi, weledi na uadilifu wanapotoa ushauri kwa viongozi huku wakizingatia maslahi mapana ya Taifa na kuepuka mambo ambayo yanaweza kusababisha mkanganyiko mkubwa miongoni mwa jamii ya watanzania na hata kusababisha migongano ya kisheria na hasara kwa Serikali.
Amesema hayo hii leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wanasheria walio katika utumishi wa umma Jijini Dodoma ulioanza tarehe 30-31 Agosti 2018.