Mkoa wa Simiyu umeweza kusajili watoto 337,662 ambao ni sawa na asilimia 91.7 ya watoto waliotarajiwa kusajiliwa kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka asilimia 5 ya watoto waliokuwa wamesajiliwa hapo awali.
Na kwa upande wa Mkoa wa Mara umeweza kusajili watoto 336,325 ambao ni sawa na asilimia 87.7 ya watoto waliotarajiwa kusajiliwa kwa kipindi cha miezi mitatu kutoka asilimia 7.1 ya hapo awali kabla ya kuanza kutekelezwa kwa mpango huo .