TARATIBU ZA MIRATHI:
1: USIMAMIZI WA MIRATHI
· Kabidhi Wasii Mkuu baada ya kuteuliwa na Mahakama au baada ya kupokea barua ya mapendekezo toka kwa Katibu Tawala anatakiwa kupeleka maombi ya usimamizi wa mirathi mahakamani.
· Kabidhi Wasii Mkuu baada ya kupewa barua ya usimamizi wa mirathi, anatakiwa kuandaa kikao cha kwanza cha utambulisho na warithi/wanufaika wote wa mirathi husika na kupokea nyaraka za umiliki wa mali zilizopimwa na ambazo hazijapimwa kutoka kwa warithi/wanufaika na taarifa ya usimamizi kutoka kwa msimamizi wa awali kama alikuwepo.
· Warithi/wanufaika kupewa fomu A.G.7 wakajaze kwenye ofisi ya Katibu Tawala ambaye marehemu alipokua anaishi au kufariki.
· Maelezo ya fomu A.G 7 yanajumuisha maelezo binafsi, maelezo ya warithi/wanufaika, maelezo ya mali za marehemu na madeni kama yapo.
· Kabidhi Wasii Mkuu atafanya upekuzi maalumu wa historia ya umiliki wa mali za marehemu kwaajili ya kuhakiki.
Utambuzi na ukaguzi wa mali za marehemu zinazohamishika na zisizohamishika.
· Kabidhi Wasii Mkuu atafanya taratibu za kuhamisha mali zilizopimwa (ardhi) toka kwenye jina la marehemu kwenda kwenye jina lake kwaajili ya usimamizi.
· Kufanya tathimini ya mali zilizotambuliwa na kuandaa kikao kuwajulisha warithi/ wanufaika kuhusu maendeleo ya usimamizi wa mirathi ya marehemu. Kikao hiki kitahusisha uhakiki wa madeni ya marehemu ikiwajumuisha warithi.
· Kuwasilisha orodha ya mali mahakamani.
· Kulipa madeni ya marehemu.
· Mgawanyo wa mali kwa warithi/wanufaika halali, kulipa madeni, ada ya usimamizi na gharama pamoja na kodi za Serikali zilizojitokeza.
· Kuwasilisha mahesabu ya mwisho Mahakamani.
· Kuhamisha umiliki wa mali toka kwenye jina la Kabidhi Wasii Mkuu kwenda kwa warithi/wanufaika halali.
· Kufungwa kwa mirathi na Kabidhi Wasii Mkuu kuondolewa kwenye usimamizi.