FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer
Miunganisho ya Wadhamini unaviwezesha vyombo visivyoshirikishwa kuwa na uwezo binafsi wa kisheria wa kufungulia na kufunguliwa shitaka katika jina la asasi, kumiliki mali na kuachia mali.
Taratibu / Mahitaji:
- Wasilisha Fomu ya Maombi TI.1 na kiambatanishi "A" ikiambatishwa na Waraka wa Katiba ya asasi unaoomba kushirikishwa (Nakala 3).
- Wasilisha picha ndogo 3 za wadhamini waliopendekezwa, na wasifa wao.
- Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambayo chombo hicho kina makao yake makuu.
- Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika sekta ya Serikali ambapo asasi inayotaka kuunganisha wadhamini wake inaangukia (kama ni asasi isiyo ya kidini).
- Wasilisha barua ya mapendekezo kutoka katika asasi kuu za kidini iwapo kinachoomba ni asasi ya kidini.
- Lipa ada halisi/ada ya sasa ni Tsh. 200,000/=.
Tanbihi:
1: Msimamizi Mkuu wa Wadhamini halazimika kuunganisha muunganisho wa Wadhamini pindi mahitaji ya hapo juu yasipotekelezwa.- Nyaraka zote zinazowasilishwa ziwe Nakala mbilimbili isipokuwa Barua ya Mapendekezo.
- Mara baada ya kuunganishwa, muunganisho huu unakuwa na wajibu ufuatao:
- Hairuhusiwi kumiliki ardhi au haki kwenye ardhi, bila kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Msimamizi Mkuu wa wadhamini (Kabidhi Wasii Mkuu).
- Kumtaarifu Msimamizi Mkuu wa wadhamini juu ya mabadiliko yoyote, mabadiliko ya wadhamini, jina la chombo, anwani ya posta, Katiba ndani ya mwezi mmoja.
- Kuwasilisha marejesho ya wadhamini kujaza fomu T.1.5 kila baada ya muda wa miezi kumi na miwili .
2: Kutaarifu juu ya mabadiliko ya jina la chombo/au marekebisho yoyote kwa ujumla.Taratibu / Mahitaji- Jaza na wasilisha Fomu ya TI.2 na TI.3.
- Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu ya mkutano uliothibitishwa ambao ulifanya mabadiliko ya jina.
- Rejesha cheti halisi cha zamani .
- Lipa ada halisi Fomu za TI. 2 na TI. 3 Tsh 50,000/=
3: Kutaarifu juu ya mabadiliko ya wadhamini.Taratibu / Mahitaji- Jaza na wasilisha Fomu ya TI. 4
- Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu za kikao rasmi ambacho kilifanya mabadiliko ya Wadhamini.
- Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
4: Marejesho ya Wadhamini.Taratibu / Mahitaji- Jaza na wasilisha Fomu ya TI.5
- Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
5: Taarifa ya kubadili anwani ya Posta.Taratibu / Mahitaji- Jaza na wasilisha Fomu ya TI.6
- Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
6:Taarifa ya kubadili Dhamana / katiba.
Taratibu / Mahitaji- Jaza na wasilisha Fomu ya TI. 7
- Lipa ada halisi (ada ya sasa ni Tsh. 50,000/=).
- Wasilisha nakala iliyothibitishwa ya kumbukumbu za kikao rasmi kilichoamua mabadiliko ya dhamana / katiba.
7.Kupata kibali cha kumiliki ardhi.
Taratibu / Mahitaji- Wasilisha barua ya maombi ukielezea matumizi yanayokusudiwa ya ardhi .
- Wasilisha nakala iliyodhibitishwa ya barua ya toleo/mkataba wa uuzaji/waraka wa ubadilishaji mmiliki.
- Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=.
8.Upekuzi wa rekodi za Wadhamini.
Taratibu / Mahitaji- Wasilisha maombi ya upekuzi.
- Lipa ada halisi ya Tsh. 50,000/=
9.Kuthibitisha nakala ya Nyaraka.
Taratibu / Mahitaji- Wasilisha maombi
- Lipa ada ya Tsh. 30,000/= ya uthibitisho wa nakala husika
10.Kupata nakala ya nyaraka
- Wasilisha maombi
- Lipa ada ya Tsh. 10,000/= kwa uthibitisho wa ofisi