MIRATHI NI NINI ?
Mirathi ni mali aliyoacha marehemu kwa ajili ya kurithishwa warithi wake halali.
Maana ingine ya Mirathi ni utaratibu unaotumiwa kuwezesha warithi waweze kugawiwa au kumilikishwa mali aliyoiacha marehemu
Sheria imeweka taratibu maalum zinazoongoza ukusanyaji, uangalizi,usimamizi,ugawaji na umiliki wa mali za marehemu baada ya kulipa madeni aliyoacha marehemu wakati wa uhai wake kama yapo na gharama zitokanazo na mazishi yake.
Aina za Mirathi
Mirathi palipo na Wosia
Mirathi ya aina hii hutokea wakati ambapo marehemu kabla ya kifo chake aliacha maandishi/matamshi au maelezo, kuhusiana na jinsi mali yake itakavyosimamiwa na hatimaye kugawanywa kwa warithi baada ya kifo chake.
Kwenye huo wosia marehemu huweza kutaja ni nani angependa awe msimamizi wa mali na/au madeni yake.
Mirathi pasipo na Wosia
i. Kusajili kifo ambapo RITA wanahusika kutoa cheti.
ii. Msimamizi kwa mujibu wa wosia atafungua shauri Mahakamani na kutoka tangazo kumthibitisha Msimamizi wa mirathi ndani ya siku 90 au pungufu ya hapo.
iii. Baada ya uteuzi msimamizi atafanya yafuatayo
iv. Kukusanya mali na madeni ya marehemu
v. Kugawa mali kwa mujibu wa wosia
vi. Kutoa taarifa za mgao Mahakamani.
Wajibu wa msimamizi wa mirathi:-
i. Kufungua shauri la maombi ya usimamizi wa mirathi
ii. Kuainisha na kutambua mali zilizoachwa na marehemu.
iii. Kulipa madeni yaliyoachwa na marehemu.
MAMLAKA NA WAJIBU WA KABIDHI WASII MKUU (RITA)
i. Kabidhi Wasii Mkuu ni kiongozi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini – RITA. Kiongozi huyu anateuliwa chini ya kifungu cha nne (4) cha sheria ya Kabidhi Wasii Mkuu (Mamlaka na Wajibu) Sura ya 27 Marejeo ya Mwaka 2002.
ii. Jukumu la msingi la nafasi hii ni kusimamia mirathi kwa kuomba kufuatia kuteuliwa na Mahakama, au kwa kuteuliwa moja kwa moja na Mahakama.
iii. Katika masuala ya usimamiaji mirathi RITA huongozwa na Sheria ya Kabidhi Wasii Mkuu (Mamlaka na Wajibu) Sura ya 27 Marejeo ya mwaka 2002.
iv. Inafaa kusema kwa maneno mengine kuwa, Ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali pamoja na mambo mengine inajishughulisha katika usimamizi wa mirathi kwenye mazingira mawili
TARATIBU AU MAZINGIRA KABIDHI WASII MKUU ANAWEZA KUSIMAMIA MIRATHI
i. Kwa maombi baada ya kupokea taarifa kutoka ofisi ya DAS au baada ya wosia kumtaja KWM kama msimamizi
ii. Kwa kuteuliwa Moja kwa Moja na Mahakama.
KWA MAOMBI
i. Kabidhi Wasii Mkuu anaweza kuombwa kusimamia Mirathi na mtu au watu wenye maslahi na mali za marehemu husika.
ii. Mtu yeyote mwenye maslahi na mali za marehemu anaweza kuomba Mahakama imteue Kabidhi Wasii Mkuu kusimamia Mirathi ya marehemu husika.
iii. Maombi ya aina hii Mahakamani ni lazima mwombaji apeleke nakala yake kwa Kabidhi Wasii Mkuu.
iv. Maombi haya yatasikilizwa kama maombi ya kawaida, na iwapo kuna pingamizi pia litasikilizwa na Mahakama itatoa maamuzi yake kama kawaida.
KUTEULIWA NA MAHAKAMA MOJA KWA MOJA
i. Iwapo Kabidhi Wasii Mkuu atateuliwa kusimamia Mirathi husika, atawajibika kukusanya mali, kulipa madeni yote halali na kugawa mali kwa wanufaika kwa mujibu wa sheria inayotumika, au waliyokubaliana warithi au kwa mujibu wa wosia kama upo.
ii. Taratibu za kuwasilisha orodha ya mali na hesabu za mwisho ataziwasilisha Mahakamani.
Usimamiaji wa mirathi RITA uongozwa na sheria zifuatazo.
UFAFANUZI WA ZIADA
Taratibu / Mahitaji
Kwa maombi
Kuteuliwa moja kwa moja na mahakama
Tanbihi: Baada ya kuteuliwa Kabidhi Wasii Mkuu atasimamia mirathi kwa kukusanya Mali, kulipa madeni na mwishoni kugawanya mali kwa warithi kulingana na sheria inayotumika au makubaliano ya wanaogawiwa, au kwa kufuata wasia, kama upo.