FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer
TOVUTI YA NDOA NA TALAKA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) ina jukumu la kusajilindoa kwa kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za ndoa nchini Tanzania nakusajili talaka kwa kuhifadhi na kutunza kumbukumbu za talakazinazopokelewa kutoka mahakamani. Usajili wa Ndoa na Talaka unasimamiwana Sheria ya Sheria ya Ndoa Sura ya 29 R.E 2019
Ili kupata huduma yetu mtandaoni mwombaji anatakiwa kujisajili kupitiatovuti yetu www.rita.go.tz na bofya menyu ya eRITA kuchaguaneno lililoandikwa Sajili hapa katika huduma za ndoa na talaka ilikujisajili kwenye mfumo.
Jinsi ya kufanya maombi:
1. MAOMBI YA SHAHADA YA KUTOKUWEPO PINGAMIZI
Ni nyaraka inayotolewa na Msajili Mkuu wa ndoa kuthibitisha kuwa raiawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hana rekodi ya ndoa na hivyo ana sifaza kuolewa nje ya nchi.
Mahitaji yanayohitajika ili kupata shahada ya Kutokuwepo pingamizi:
- Cheti cha kuzaliwa na pasipoti ya mwombaji,
- Barua ya uthibitishaji kutoka kwa mzazi/mlezi,
- Kitambulisho cha mzazi/mlezi
- Pasipoti/kitambulisho cha mtarajiwa anayekusudiwa
Jinsi Maombi yanavyofanyika
- Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kujaza fomu ya maombi ya mtandaoni (RGM12), maombi yakishatumwa mtandaoni, mfumo utatoa namba ya malipo na mwombaji atafanya malipo. Gharama ni Tsh 300,000/=
- Waombaji watajulishwa kupitia akaunti yao ikiwa maombi yao yamekubaliwa au kukataliwa, Wanaweza pia kufuatilia hali ya maombi yao kupitia mfumo wa mtandaoni.
2. MAOMBI YA LESENI YA KUFUNGISHA NDOA.
Leseni ya kufungisha ndoa ni hati inayotolewa na Msajili Mkuu wa Ndoaikimpa kiongozi wa dini mamlaka ya kufungisha ndoa. Msajili Mkuuanaweza kufuta leseni ya kufungisha ndoa wakati wowote kwa chapishola kwenye Gazeti la Serikali
Jinsi ya kufanya maombi
- Mwombaji atajaza fomu ya maombi ya mtandaoni (RGMF 2) na kuambatisha nyaraka kuambatisha zifuatazo:
- kitambulisho cha kitaifa au
- kitambulisho cha kura
- pasipoti na
- picha.
- Sharti la awali la kusajiliwa ni kwa Mwakilishi wa Taasisi ya Dini kusajiliwa katika mfumo wa RITA.
- Mfumo utatoa namba ya malipo kwa Mwombaji na Mwombaji atalipa ada ya maombi. Malipo ni Tsh 60,000/=
3. KIBALI MAALUM CHA MSAJILI MKUU
Msajili Mkuu anaweza kutohitaji taarifa ya kutangaza nia ya kufungandoa kama matakwa ya Sheria ya Ndoa inavyotaka pale ambapo kuna sababuya kutosha ya kutotangaza nia kwa kufanya maombi kwa kuambatisha nyarakazinazohitajika.
Jinsi ya kufanya maombi:-
- Mwombaji atafanya maombi mtandaoni na kuweka ushahidi wa nyaraka juu ya sababu za kwa nini anakwepa kutangaza nia ya siku 21 ya kuoa.
- Maombi yanaweza kukubaliwa au kukataliwa
- Malipo yatafanywa baada ya maombi kukubaliwa na kulipiwa pesa ya Tsh 200,000/=
- Kibali kitatolewa
4. MAOMBI YA KIBALI CHA KUFUNGA NDOA MAHALI MAALUM
Msajili Mkuu anaweza kutoa kibali cha kufunga ndoa mahali maalumtofauti na mahali palipozoeleka kutumika kama mahali pa ibada aumikusanyiko baada ya kupokea maombi ya mwenzi wanaotegemea kuoana.
Jinsi ya kufanya maombi:-
- Mwombaji atafanya maombi mtandaoni kupitia eRITA na kuendelea kujaza fomu na kuambatisha nyaraka. Mwombaji lazima aeleze mahali alipokusudia kufungia ndoa yake na kutuma fomu ya maombi mtandaoni na nyaraka za kuthibitisha maombi.
- Mwombaji atalipia Tsh 200,000/=
- Kibali kitatolewa.
5. MAOMBI YA KIBALI CHA KUTOKUWA NA NDOA
Ni hati inayotolewa na Msajili Mkuu kuthibitisha kuwa muombaji wa hatihiyo kuwa hana ndoa.
Jinsi ya kufanya Maombi:-
- Mwombaji atume maombi mtandaoni kwa kujaza fomu ya maombi ya mtandaoni (RGM12), maombi yakishatumwa mtandaoni, mfumo utatoa namba ya malipo na mwombaji atafanya malipo.
- Waombaji watajulishwa kupitia akaunti yao ikiwa maombi yao yamekubaliwa au kukataliwa, Wanaweza pia kufuatilia hali ya maombi yao kupitia mfumo wa mtandaoni.
- Kibali kitatolewa baada ya kulipia Tsh 200,000/=
6. USAJILI WA NDOA ZILIZOFUNGWA NJE YA NCHI
Msajili Mkuu ana mamlaka ya kusajili ndoa zilizofungwa nje ya nchi.
Jinsi ya kufanya Maombi:-
- Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zifuatazo:-
- cheti cha ndoa kilichothibitishwa na ubalozi wa nchi husika
- pasi za kusafiria za wanandoa
Cheti kitakachoambatishwa kama hakikuandikwa kwa lugha ya Kiingereza auKiswahili kinapaswa kiambatanishwa na tafsiri iliyothibitishwa kwakiingereza au kiswahili na afisa ubalozi wa nchi kinapotoka au na BAKITAkwa Tanzania.
- Mwombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh 200,000/=
- Cheti kitatolewa.
7. TALAKA
Huduma ya talaka hutolewa kwa mujibu wa sheria ya ndoa kwa kutoa cheticha talaka.
Mahitaji yanayohitajika ili kufanya maombi ya cheti cha talaka
- Hukumu
- Hati ya Talaka
- Cheti cha ndoa
Jinsi ya kufanya maombi
- Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zitakazohitajika kwenye mfumo
- Muombaji atajulishwa kupitia akaunti yake ikiwa maombi yake yamekubaliwa au kukataliwa,
- Muombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh 40,000/=
- Cheti cha Talaka kitatolewa.
8. TALAKA ILIYOTOLEWA YA NCHI
Maamuzi ya mashauri ya ndoa yaliyotolewa na mahakama zenye mamlaka zanchi za nje yatatambulika na kusajili nchini. Tanzania.
Mahitaji yanayohitajika ili kufanya maombi
- Hukumu ya kuvunja ndoa/ kubatilisha
- Hati ya talaka ambapo haki ya kukata rufaa haipo tena na iwapo haikuandikwa kwa lugha ya Kiingereza au kiswahili inapaswa iambatanishwa na tafsiri iliyothibitishwa kwa kiingereza au kiswahili na afisa ubalozi wa mamlaka husika.
- Cheti cha ndoa
Jinsi ya kufanya maombi
- Mwombaji atatuma maombi kwa njia ya mtandao kupitia tovuti - www.rita.go.tz maombi yatafanywa kwa kuambatisha nyaraka zitakazohitajika kwenye mfumo
- Mwombaji katika maombi yake lazima aainishe ni mahakama ya nchi gani iliyotoa hiyo talaka.
- Muombaji atalipia gharama inayotakiwa ya Tsh. 200,000/=
- Cheti cha Talaka kitatolewa.