RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
September
18
2024
No title
News & Update
JAFARI MALEMA
`
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi amekutana na viongozi wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini RITA kuweka mikakati ya kuongeza kiwango cha usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu, matukio hayo ni vizazi, vifo na sababu zake, ndoa, talaka na watoto wa kuasili.
Kupitia wasilisho maalum la mikakati ya wakala, Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA Bw. Frank Kanyusi amesema Tanzania imekuwa mfano wa kuigwa na nchi mbalimbali za Afrika kutokana na kupiga hatua katika mifumo na sheria za usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu.
" Sisi kama nchi tumekuwa tukipata nafasi ya kuwasilisha mafanikio yetu wakati wa vikao vya nchi za Afrika ( Africa CRVS Summit) kuhusu usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu, pia baadhi ya nchi hizo zimefika Tanzania kujifunza kupitia mafanikio hayo, nchi hizo ni Ethiopia, Sierralion na Uganda". Alisema Bw. Kanyusi.

Tags : #Legal News

View Full Page