RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
September
11
2024
No title
News & Update
JAFARI MALEMA
`
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) umeshiriki hafla ya kubadilishiana hati ya ushirikiano na Bodi ya Mikopo wa Elimu ya Juu (HESLB) leo Septemba 11, 2024. Jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi Kabidhi Wasii Mkuu Bw. Frank Kanyusi amesema RITA inafanya kazi na kushirikiana na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kupitia uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa na vifo vya wazazi wa wanafunzi kisha kupatiwa verification code ambayo inatumika kuunganisha taarifa ya uhalali wa nyaraka husika.
Hafla hiyo ilijumuisha taasisi zinazohusika na masuala ya utambuzi ambazo ni Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini - RITA, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa -NIDA na Taasisi ya Credit info LTD.
“Kutokana na agizo la Serikali kuzitaka taasisi hizi mifumo yake kusomana sisi kama RITA tumefanikisha kila mwananchi anayehitaji huduma Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu HESLB, NIDA, Uhamiaji na NHIF kupata verification code na kuwasilisha katika taasisi husika".

Tags : #Registration

View Full Page