Notice: Undefined offset: 0 in /home/ritaag/public_html/new/news.php on line 38

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/ritaag/public_html/new/news.php on line 38
Usajili wa wanafunzi katika shule za msingi manispaa ya Kinondoni, 6-18BRI.
RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
MEDIA CENTRE
February
19
2015
Usajili wa wanafunzi katika shule za msingi manispaa ya Kinondoni, 6-18BRI.
News & Update
`

 

TAARIFA KWA UMMA

 

WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI KINONDONI KUSAJILIWA NA KUPATA VYETI VYA KUZALIWA MASHULENI.

 

Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA)         unategemea kuanza rasmi mkakati wa kuwasajili na kuwapa vyeti vya kuzaliwa wanafunzi wa shule za Msingi za Manispaa ya kinondoni Ijumaa wiki hii ambapo mpango huu utatekelezwa katika shule 140 zenye wanafuzi wapatao 155,944. Lengo ni kusajili wanafunzi 20,000.

Kuzinduliwa kwa mkakati huu katika Manispaa ya Kinondoni ni muendelezo wa mkakati mkuu uliozinduliwa Mwezi Aprili 2014 unaowawezesha wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari kusajiliwa na kupata vyeti vya Kuzaliwa katika shule wanazosoma.

Katika mkakati huu kila shule huteua mwalimu mmoja atakayeratibu zoezi  baada ya kupewa mafunzo ya kina kuhusu Usajili wa Vizazi na kupewa vitendea kazi kwa ajili ya kufanya usajili wa awali katika shule zao. Baada ya Mwalimu kuwatangazia wanafunzi na wazazi kuhusu huduma hiyo kupatikana shuleni atagawa fomu za maombi wa wanaohitaji na atahakiki fomu zilizojazwa na atazikusanya na kuziwasilisha fomu RITA kwa ajili ya kuhakikiwa na kuandaliwa vyeti. Mara baada ya vyeti kukamilishwa hupelekwa kwa mwalimu ambaye atavigawa kwa wanafunzi husika.

Tayari mkakati huu umeshaanza kutekelezwa katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam umeshafanyika katika shule  105 za Msingi na  96 za Sekondari za Manispaa ya Ilala na kuonyesha mafanikio Makubwa na Zaidi ya wanafunzi 16,000 wamesajiliwa na kupata Vyeti vya kuzaliwa. Kati ya hao 51.2% Ni wavulana na  48.8%  ni wasichana. Usajili katika manispaa ya Ilala bado unaendelea.

Chimbuko la Mkakati huu ni uhitaji mkubwa wa Nyaraka hii Kutokana na mfumo wa Elimu kusisitiza Cheti cha kuzaliwa kuwa nyaraka inayothibitisha umri wa mwananfunzi mara anapotoka hatua moja ya elimu kwenda inayofuata.

Baada ya kukidhi vigezo mwanafunzi hupata cheti kwa kufuata mfumo wa kawaida wa uhakiki ili kuhakikisha ni wale wanaostahili tu ndio wanaopata vyeti vya kuzaliwa. Wanafunzi watakaosajiliwa ni wale waliozaliwa katika Mkoa wowote wa Tanzania Bara  na watatakiwa kuwa na viambatanisho kama Tangazo la Kizazi, kadi ya Kliniki, Cheti cha Ubatizo, Cheti cha Falaki, Pasi ya kusafiria na watakaokosa vyote kati ya vilivyotajwa kutakuwa na utaratibu maalumu utakaowekwa ili kuwawezesha nao kupata cheti cha kuzaliwa.

RITA inaamini wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule za Msingi katika Manispaa ya Kinondoni watatumia fursa hii kuwasajili watoto ili wapate vyeti vya kuzaliwa. Cheti cha kuzaliwa ni nyaraka muhimu kwa kila mwananchi kwani humwezesha mwanafunzi kuweza kupata nafasi za masomo ya sekondari na baadae elimu ya juu, kupata mikopo ya elimu, kufungua akaunti ya Benki, kupata huduma za Afya kupitia mifuko ya jamii, kupata pasi ya kusafiria na matumizi mengineyo.

View Full Page