RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
`
Usimamiaji Mirathi
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

RITA husimamia mirathi ama kwa kuombwa kukifuatia kuteuliwa na mahakama, au kwa kuteuliwa moja kwa moja na mahakama. Katika masuala ya usimamiaji mirathi RITA uongozwa na sheria zifuatazo.

Taratibu / Mahitaji

Kwa maombi

  • Wasilisha barua ya maombi RITA au Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) katika wilaya inayohusika ambayo marehemu ana mali, ambapo DAS atajaza Fomu na kuwasilisha RITA akiomba Kabidhi Wasii Mkuu kusimamia mali za marehemu huyo. Mwombaji awe mtu ana cha kupoteza endapo mirathi haitasimamiwa.
  • Kabidhi Wasii Mkuu atachambua maombi na akiyaona yanafaa kwa kusimamia mali ataiomba mahakama imteue kuwa msimamizi wa mirathi husika vinginevyo atawashauri wahusika njia mbadala ya kuitumia.
  • Lipa ada ya mwanzo ya kusimamia kulingana na ukubwa wa mali .

Kuteuliwa moja kwa moja na mahakama

  • Mtu yeyote mwenye uchungu na mali za marehemu anaweza kuomba mahakama imteue Kabidhi Wasii Mkuu kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu anayehusika. Kabili Wasii Mkuu apatiwe nakala za maombi.
  • Mahakama itasikiliza maombi na kufanya uteuzi kama inavyoona inafaa.

Tanbihi: Baada ya kuteuliwa Kabidhi Wasii Mkuu atasimamia mirathi kwa kukusanya Mali, kulipa madeni na mwishoni kugawanya mali kwa warithi kulingana na sheria inayotumika au makubaliano ya wanaogawiwa, au kwa kufuata wasia, kama upo.

Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu