RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
USAJILI
`
Kizazi
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

1: Usajili wa kizazi ndani ya siku 90

  • Kama kizazi kimetokea hospitalini,kituo cha afya au zahanati hakikisha unapatiwa Tangazo la kizazi kabla ya kuondoka.
  • Endapo kizazi kitakuwa kimetokea nyumbani,toa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa kijiji au Msajili wa vizazi au vifo wa wilaya ili ipatiwe tanzazo la kizazi.taarifa hii itolewe ndani ya siku 90.
  • Ingia katika mfumo wa eRITA https://erita.rita.go.tz/auth chagua lugha unayopenda kutumia kisha jisajili kwaajili ya kupata akaunti ya kuingilia katika mfumo
  •  ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza kizazi nenda mbele ubonyeze cheti kipya halafu jaza taarifa za mtoto kwa usahihi
  •  Hakikisha umescani tangazo la mtoto kwaajili ya kuliambatanisha baaada ya kujaza taarifa za mtoto.
  • Mfumo utatoa kumbukumbu ya malipo ya Shs.8,000 itumie kufanya malipo katika mitandao ya simu kwa kuchagua huduma za serikali

2: Usajili nje ya siku 90 lakini chini ya miaka 10.

  • Ingia katika mfumo wa eRITA https://erita.rita.go.tz/auth chagua lugha unayopenda kutumia kisha jisajili ili upate akaunti ya kuingilia katika mfumo.
  • ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza Kizazi nenda mbele ubonyeze cheti kipya halafu jaza taarifa za mtoto kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti chako
  •  Hakikisha umescani nyaraka zako kwaajili ya kuziambatanisha baaada ya kujaza taarifa za mtoto nyaraka hizo ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
  • Mfumo utatoa kumbukumbu ya malipo ya Shs 8,000 itumie kufanya malipo katika mitandao ya simu kwa kuchagua huduma za serikali
  • Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa ukiona neno approved au issued jua kuwa cheti chako kiko tayari na ukiona kuna ujumbe unatoa maelekezo hakikisha unayafuata ili maombi yako yapitishwe

3: Kuandikisha kizazi kilichochelewa kuandikishwa zaidi ya miaka 10

  • Ingia katika mfumo wa eRITA https://erita.rita.go.tz/auth chagua lugha unayopenda kutumia kisha jisajili ili upate akaunti ya kuingilia katika mfumo.
  • ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza kizazi nenda mbele ubonyeze cheti kipya halafu jaza taarifa za mtoto kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti chako
  •  Hakikisha umescani nyaraka zako kwaajili ya kuziambatanisha baaada ya kujaza taarifa za mtoto nyaraka hizo ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
  • Mfumo utatoa kumbukumbu ya malipo ya Shs 20,000 itumie kufanya malipo katika mitandao ya simu kwa kuchagua huduma za serikali
  • Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa ukiona neno approved au issued jua kuwa cheti chako kiko tayari na ukiona kuna ujumbe unatoa maelekezo hakikisha unayafuata ili maombi yako yapitishwe

4: Kubadilisha muonekano wa cheti cha zamani cha kuchapa na kupata kipya cha kieletronic

  • Ingia katika mfumo wa eRITA https://erita.rita.go.tz/auth chagua lugha unayopenda kutumia kisha jisajili ili upate akaunti ya kuingilia katika mfumo.
  • ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza kizazi nenda mbele ubonyeze cheti cha zamani kuwa kipya halafu jaza taarifa za mtoto kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti chako
  •  Hakikisha umescani cheti chako cha zamani na nyaraka zako kwaajili ya kuziambatanisha baaada ya kujaza taarifa zako nyaraka hizo ni :-passipoti, cheti cha kumaliza elimu ya msingi, sekondari, kadi ya kliniki,cheti cha ubatizo(kama unahusika),barua kutoka ofisi za serikali zinazohusika kama ofisi ya mtendaji wa kata;mtendaji wa kijiji.
  • Mfumo utatoa kumbukumbu ya malipo ya Shs 8,000 itumie kufanya malipo katika mitandao ya simu kwa kuchagua huduma za serikali
  • Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa ukiona neno approved au issued jua kuwa cheti chako kiko tayari na ukiona kuna ujumbe unatoa maelekezo hakikisha unayafuata ili maombi yako yapitishwe

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa

  • Kufanya masahihisho kwenye cheti cha kuzaliwa
  •  Ambatanisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako – barua inayotetea ombi lako na kiambatanisho(cheti cha ubatizo,kadi ya clinic au vyeti vya shule na vielelezo vingine msajili atakavyohitaji kwaajili ya kujiridhisha, vielelezo vya wazazi kama vile cheti cha kuzaliwa, vyeti vya vifo au vitambulisho vyao  ikiwa jina la mmoja wa wazazi limekoseewa)
  • Rejesha cheti kinachotakiwa kusahihishwa.
  • Ada baada ya ombi lako kukubaliwa (ada ya sasa ni Tsh 13,000/= )
Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu