RITA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
USAJILI
`
Kifo
FRANK KANYUSI FRANK
Administrator General And Chief Executive Officer

1: Usajili wa kifo ndani ya siku 30

  • Iwapo kifo kimetokea hospitalini, kwenye kituo cha afya au katika zahanati, hakikisha unapata Kibali cha Mazishi. Ikitokea kifo kimetokea nyumbani toa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji, au kwa Msajili wa Wilaya kupata kibali cha mazishi. Jambo hili lifanyike ndani ya siku 30.
  • Ingia katika mfumo wa eRITA https://erita.rita.go.tz/auth chagua lugha unayopenda kutumia kisha jisajili ili upate akaunti ya kuingilia katika mfumo.
  • Ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza huduma za vifo nenda mbele bonyeza cheti kipya halafu jaza taarifa za marehemu kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti
  • Hakikisha umescani nyaraka zako na kibali cha mazishi cha marehemu. nyaraka hizo ni :- NIDA ya marehemu,kadi ya kura ya mrehemu, pasi yakusafiria ya marehemu,cheti cha kuzaliwa cha mtoto wa marehemu au cheti cha ndoa chamke au mume wa marehemu
  • Mfumo utatoa kumbukumbu ya malipo ya Shs 7,000 itumie kufanya malipo katika mitandao ya simu kwa kuchagua huduma za serikali
  • Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa ukiona neno approved au issued jua kuwa cheti chako kiko tayari na ukiona kuna ujumbe unatoa maelekezo hakikisha unayafuata ili maombi yako yapitishwe

2: Usajili wa kifo uliochelewa

  • Ingia katika mfumo wa eRITA https://erita.rita.go.tz/auth chagua lugha unayopenda kutumia kisha jisajili ili upate akaunti ya kuingilia katika mfumo.
  • ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza huduma za Vifo nenda mbele bonyeza cheti kipya halafu jaza taarifa za marehemu kwa usahihi na kuchagua sehemu utakayo chukua cheti
  • Hakikisha umescani nyaraka zako na kibali cha mazishi cha marehemu nyaraka za kuthibitisha (kumbukumbu za kikao cha familia na Barua kutoka kwenye mamlaka za serikali zinazohusika mfano Kata, Ofisa Mtendaji, Ofisa Mtendaji wa Kijiji) kuthibitisha kifo hicho pamoja na NIDA ya marehemu,kadi ya kura ya mrehemu, pasi yakusafiria ya marehemu,cheti cha kuzaliwa cha mtoto wa marehemu au cheti cha ndoa chamke au mume wa marehemu
  • Mfumo utatoa kumbukumbu ya malipo ya Shs 20,000 kama ni kifo zaidi ya siku 30 nani zaidi ya miaka 10 itumie kufanya malipo katika mitandao ya simu kwa kuchagua huduma za serikali
  • Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa ukiona neno approved au issued jua kuwa cheti chako kiko tayari na ukiona kuna ujumbe unatoa maelekezo hakikisha unayafuata ili maombi yako yapitishwe

3: Uthibitisho wa Vyeti vya vifo

  • Ingia katika mfumo wa eRITA https://erita.rita.go.tz/auth chagua lugha unayopenda kutumia kisha jisajili ili upate akaunti ya kuingilia katika mfumo.
  • ingia katika mfumo wa eRITA na kisha bonyeza uhakiki halafu jaza taarifa za marehemu kwa usahihi
  • Hakikisha umescani cheti cha marehemu na kasha ukiambatanishe katika mfumo
  • Mfumo utatoa kumbukumbu ya malipo ya Shs 6,000
  • Baada ya kukamilisha kutuma maombi unashauriwa kutembelea akaunti yako kufuatailia kama yamepitishwa ukiona neno approved au issued jua kuwa cheti chako kiko tayari na ukiona kuna ujumbe unatoa maelekezo hakikisha unayafuata ili maombi yako yapitishwe

4: Usajili wa Kifo kilichotokea nje ya nnchi

  • Wasilisha nakala ya cheti cha kifo kutoka nnchi kifo kilipotokea.
  • Pasi ya kusafiria ya marehemu
  • Taarifa /cheti cha matibabu
  • Barua kutoka Ubalozi wa Tanzania  wa nnchi kifo kilipotokea ya kutaarifu RITA kifo hicho.
  • Kitambulisho cha Mtoa taarifa
  • Lipa ada inayotakiwa (ada ya sasa ni Tsh. 30,000/=).

5: Kufanya masahihisho kwenye cheti

  • Wasilisha maombi ya masahihisho.
  • Ambatisha nyaraka za kuunga mkono ombi lako.
  • Wasilisha cheti kinachotakiwa kufanyiwa masahihisho.
  • Lipa ada inayotakiwa pale maombi yanapokubalika (ada ya sasa ni Tsh. 13,000/=).

Ona Ukurasa Kamili
Washirika wetu
Wadau Wetu