RITA
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Registration Insolvency and Trusteeship Agency
MEDIA CENTRE
August
05
2024
WANANCHI WACHANGAMKIA FURSA YA VYETI VYA KUZALIWA NANENANE DODOMA
News & Update
`
Wananchi Jijini Dodoma leo Agosti 05, 2024 wameendelea kujitokeza na kupatiwa huduma katika banda la RITA kwenye maonesho ya Wakulima nanenane Jijini Dodoma.
Akielezea utaratibu wa kusajili vizazi na vifo, Afisa Usajili Bw. Mwinyijuma Moshi amesema RITA imerahisisha utoaji wa huduma kupitia mfumo wa kielektroniki wa eRITA ambapo mwananchi anaweza kutuma maombi yake popote alipo kwa kutumia simu janja au kopyuta.
" Mwananchi anaweza kutuma maombi akiwa nyumbani au sehemu yoyote kupitia simu yake au kompyuta kwa kuingia katika tovuti yetu www.rita.go.tz kisha kubonyeza kitufe kilichoandikwa eRITA na kufuata maelekezo, pia wakati anajaza akumbuke kuchagua kituo cha kuchukulia ambacho ni nanenane na atapata cheti chake ndani ya masaa 24 wakati huu wa maonesho". Alisema Mwinyijuma.
Huduma zinazotolewa katika kipindi chote cha maonesho hayo ya nanenane ni pamoja na elimu ya kina kuhusu huduma mbalimbali za Wakala, usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa na vifo, kuandika na kuhifadhi wosia, msaada wa kisheria bure kuhusu
masuala ya mirathi.
View Full Page